Mwanariadha kutoka Uganda Rebecca Cheptegei afariki kwa kuchomwa moto na Mpenzi wake

-rickmedia: Saraphina Jerry

Saraphina Jerry

4 months ago
rickmedia: mwanariadha-kutoka-uganda-rebecca-cheptegei-afariki-kwa-kuchomwa-moto-mpenzi-wake-820-rickmedia

Mwanariadha wa Uganda na Mshiriki wa Michezo ya Olimpiki, Rebecca Cheptegei amefariki dunia kutokana na majereha aliyopata baada ya kuchomwa Moto na mpenzi wake.

Cheptegei alihamishiwa Nchini Kenya kwaajili ya Matibabu zaidi huku taarifa zikieleza sababu ya mpenzi wake kummwagia Petroli na kumchoma moto ni Mgogoro wa Ardhi.

Kabla ya kifo chake, Mwanariadha huyo alishiriki Mbio za Olimpiki jijini Paris 2024 na kushika nafasi ya 44, pia, aliwahi kushika nafasi ya 14 katika Mbio za Michuano ya Mabingwa wa Dunia mwaka 2023.