Timu ya Taifa ya Tanzania ‘Taifa Stars’ imeambulia pointi moja katika matokeo ya 0-0 ya mchezo wa kwanza wa Kundi H dhidi ya Ethiopia kwenye kuwania Kufuzu Michuano ya Afrika (AFCON 2025), wakitoana jasho kwenye Uwanja wa Mkapa, Dar es Salaam.
Baada ya matokeo hayo mchezo unaofuata ni dhidi ya Guinea (Septemba 10, 2024) ambapo utachezwa kwenye Uwanja wa Charles Konan Banny, Nchini Ivory Coast ambapo Guinea wamechagua kutumia kama Uwanja wao wa Nyumbani.
Timu mbili zitakazoongoza Kundi zitafuzu kucheza michuano hiyo ambayo inatarajiwa kufanyika Nchini Morocco.