Chris Brown aamrishwa kulipamkopo wa zaidi ya Tsh.Bilioni 4

-rickmedia: Saraphina Jerry

Saraphina Jerry

1 year ago
rickmedia: chris-brown-aamrishwa-kulipamkopo-zaidi-tshbilioni-150-rickmedia

Mahakama ya mjini Los Angels imemuamuru Staa wa muziki Chris Brown kulipa deni la $1.7M- Tsh.Bilioni 4.3+ alizokopa katika benki ya City National kwa ajili ya kununua migahawa miwili ya Popeyes Chicken.

Staa huyo licha kuchukua mkopo huo kwa ajili ya kununua migahawa hiyo hakufanya hivyo na alishindwa kulipa deni hilo, Kwa Mujibu wa vyombo vya Habari Chris Brown ni lazima alipe deni hilo kutokana na kesi iliyofunguliwa na Benki hiyo Mjini Georgia ambapo alishtumiwa kwa kushindwa kutimiza ahadi yake inayohusiana na uwekezaji..

Breezy ana siku 30 pekee za kujibu na kukamilisha taratibu zote za deni hilo na endapo atashindwa basi atakuwa hatarini kupoteza vitu vyake vya thamani kama Nyumba na mali zake nyingine.

.