AI inavyokuja kuwapa changamoto wasanii wa muziki Duniani

-rickmedia: Saraphina Jerry

Saraphina Jerry

16 hours ago
rickmedia: inavyokuja-kuwapa-changamoto-wasanii-muziki-duniani-715-rickmedia

Akili Bandia 'AI' inakuja kwa kasi Duniani na watu wengi wanapoteza ufanisi katika sekta mbalimbali(Hawafikirii kwa kina) kwani kwenye kazi zao nyingi hutumia akili badia 'AI' kupata majibu kitu kinachodhoofisha namna yao ya kufikiri kwani wanajua majibu wanakoyapata kiurahisi, kwenye muziki hiki kimekuwa ni kilio kikubwa mno 'AI'.

Kwa hapa kwetu nchini Tanzania tayari kuna nyimbo kadhaa ambazo zinasikika sana (Zina-Tren) ambazo zimetengenezwa kwa AI ni nyimbo za Injili (Gospel) na watu wanazipenda sana japo wengi wao hawajajua kama nyimbo hizo hazijaimbwa na watu halisi bali ni akili bandia 'AI'.

Kwanza nyimbo hizo zinasikika vizuru na ukimsikiliza msanii unasikia namna ambavyo amepangilia sauti hakika lazima ufurahie muziki huo, kuna nyimbo kama 'Nitaamini' wImbo wa 'Voice of hope' na 'Mengi kwa ajili yangu' zote zikiwa zimeandaliwa na Emanuel Nicarios na bado kuna nyimbo nyingine nyingi tofauti na hizi.

Kwa ukuaji huu wa teknoloji kuna haja ya kila mtu kufanya kazi yake kwa umakini kwani kwa upande wangu huwa nasema (Kupitia AI ni suala la muda tu ila kila mtu itampa chngamoto kwenye kazi yake.