Sean Kingstone Anakabiliwa na Mashtaka 10, Mama Yake 8

-rickmedia: Lanka Ting

Lanka Ting

9 months ago
rickmedia: sean-kingstone-anakabiliwa-mashtaka-10-mama-yake-903-rickmedia

Kulingana na agizo la kukamatwa lililotolewa katika Kaunti ya Broward mwimbaji #SeanKingstone anakabiliwa na jumla ya mashtaka 10 yanayohusiana na udanganyifu huku kubwa zaidi likiwa ni njama iliyopangwa ya kulaghai kampuni kadhaa.

Mamlaka zinasema #Sean na mama yake, #JaniceTurner walichukua vito vyenye thamani ya hadi $480K- Tsh.Bilioni 1.2+ huku ulaghai mwingine unaodaiwa kuwa wameufanya ni kukwepa kulipa gari aina ya #CadillacEscalade lenye thamani ya $159,701.49- Tsh.Milioni 416+.

#Sean pia anakabiliwa na shtaka kubwa la kushindwa kulipa kitanda alichotengenezewa chenye thamani ya $86,568.33- Tsh. Milioni 225+, Mashtaka mengine yote yanahusiana na kulaghai benki na kuandika hundi feki. #Janice anakabiliwa na jumla ya mashtaka 8.