Msanii wa Muziki wa Rap kutoka Marekani Ambaye Ni Hit-Maker Wa Ngoma Ya Watch Me/ Nae Nae’ Amehukumiwa Kifungo Cha Miaka 30 Jela Kwa Mauaji Ya Binamu Yake ‘Frederick Rooks III’ 2021.
Silento (27) Ambaye Jina Lake Halisi Ni ‘Rick Lamar’, Alikiri Kuwa Alifanya Mauaji Hayo Bila Kukusudia Lakini Alikuwa Na Matatizo Ya Akili, Pamoja Na Mashtaka Mengine Kama Kumiliki Silaha N.k. Hukumu Ya Kesi Ya Rapa Huyu Imetolewa Leo Na Jaji Wa Atlanta .
Kumbuka Tukio la Mauaji lilitokea Januari 21 katika eneo la Panthersville ambapo polisi walifika eneo la tukio baada ya kupigwa simu saa 3:30 asubuhi, baada ya kufika Walikuta Frederick Rooks amekufa eneo la tukio akiwa na majeraha mengi ya risasi Mwilini. (Kwa Mujibu Wa Polisi Wa DeKalb “Rod Bryant”). Hivyo Baada Ya Upelelezi Wa Kina Idara Ya Polisi Ya Dekalb Walibaini Hawk (Silento) Ni Binamu Wa Rooks Na Ndio Anayehusika Na Mauaji Ya Rooks Baada Ya Majirani Kudai Alioneoana Akikimbiza Gari Kwa Kasi Baada Ya Kufanya Tukio Hilo.
Hata Hivyo Baada Ya Hukumu Hiyo, Team Ya Silento Imetoa Ujumbe Uliomnukuu Silento Akiwaomba Radhi Mashabiki Zake Na Kuwaahidi Kuwa Ataendelea Kufanya Muziki Akiwa Gerezani. Silento Pia Amesema Kwamba ‘Siwezi Kurudisha Muda Nyuma, Ila Naweza Kutumikia Muda Niliohukumiwa Kisheria.