Ni takribani wiki mbili zimepita toka avunjiwe duka lake la Simu lililopo Sinza Jijini Dar es Salaam, mwanamuziki Billnass kwa mara ya kwanza ameonesha baadhi ya simu na laptop zilizoharibiwa vibaya kwa moto uliochomwa na waandamanaji dukani hapo.
Kupitia akaunti yake ya Snapchat Billnass ameweka video hii chini >>>>>>>>>
Billnass ni kati ya wasanii waliolengwa na waandamanaji walioandamana siku ya uchaguzi Mkuu October 29,2025 kwa kile walichokiita mwanamuziki huyo kujihusisha na siasa upande wa Chama tawala (CCM). Wasanii wengine walioharibiwa biashara zao ni pamoja na Jux na Shilole