Rais wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan kesho Ijumaa, Novemba 14, 2025 saa 4:00 asubuhi, Ikulu ya Chamwino mkoani Dodoma atamwapisha Dk Mwigulu Nchemba kuwa Waziri Mkuu.
Ni baada ya leo Alhamisi, Rais Samia kumteua Dk Mwigulu ambaye ni Mbunge wa Iramba Magharibi (CCM), Mkoa wa Singida kuwa Waziri Mkuu na kuthibitishwa na Bunge kushika wadhifa huo.
Pia, kesho Ijumaa, saa 9 alasiri, Rais Samia atatoa hotuba yake ya kulizindua Bunge la 13 jijini Dodoma