Rais Kagame akanusha kumuandaa binti yake kuja kuwa Rais wa Rwanda

-rickmedia: Saraphina Jerry

Saraphina Jerry

2 days ago
rickmedia: rais-kagame-akanusha-kumuandaa-binti-yake-kuja-kuwa-rais-rwanda-610-rickmedia

Rais wa Rwanda, Paul Kagame, amepinga madai kuwa anamuandaa mtoto wake "Ange Kagame" kuwa mrithi wa kiti cha urais.

Akizungumza mjini Kigali, Kagame alisema watoto wake ni Wanyarwanda kama wengine na wanapaswa kuishi maisha ya kawaida Amesisitiza kuwa hawezi kumpangia mtu urais, akiongeza kuwa hata binti yake anayehusishwa na madai hayo huenda hana nia ya kuingia siasani.

Rais Kagame ameongoza Rwanda kwa miaka mingi, akiendelea kujenga taifa hilo baada ya kipindi kigumu cha mauaji ya halaiki.