Daktari wa miaka 100 anayeendelea kupiga kazi kama kawaida

-rickmedia: Rick

Rick

8 hours ago
rickmedia: daktari-miaka-100-anayeendelea-kupiga-kazi-kama-kawaida-860-rickmedia

Kutana na Daktari Teru Kasamatsu mwenye umri wa miaka 100 ambaye hadi sasa anaendelea na kazi hiyo kwenye hospitali ya familia huko Japan.

Teru Kasamatsu anasema kuwa siri ya kufikisha miaka 100 huku akiwa bado anaweza kufanya kazi zingine za kijamii ni kuwa na utaratibu mzuri wa maisha kama kula kwa mpangile mzuri na mazoezi ya kutosha.

Teru Kasamatsu hufanya kazi kwenye Hospitali hiyo ya familia kwa siku tatu tu ndani ya wiki. Kwa mujibu wake anasema alisomea udaktari kutokana na ushauri aliopewa na baba yake wakati anasoma Elimu ya juu.