Trump asikitishwa na vikwazo kwenye jitihada zake za kumaliza vita ya Ukraine

-rickmedia: Saraphina Jerry

Saraphina Jerry

6 hours ago
rickmedia: trump-asikitishwa-vikwazo-kwenye-jitihada-zake-kumaliza-vita-ukraine-237-rickmedia

Rais wa Marekani Donald Trump ameonyesha masikitiko kufuatia kushindikana kwa juhudi zake za kumaliza vita vya Ukraine.

Amesema licha ya mawasiliano ya mara kwa mara na Rais Vladimir Putin, juhudi hizo hazijazaa matunda. Kauli hiyo imekuja baada ya Marekani kutangaza vikwazo vipya vya kiuchumi dhidi ya Urusi, vikihusisha kampuni mbili kubwa za mafuta.

Aidha, Trump ametangaza kuahirishwa kwa muda usiojulikana kwa mkutano wake na Putin uliokuwa umepangwa kufanyika Budapest, Hungary.