Mwanasiasa nchini Kenya, Martha Karua ametangaza nia ya kugombea Urais mwaka 2027 kupitia Party of Liberal Progressives (PLP), huku akiahidi kutumikia muhula mmoja pekee iwapo ataibuka mshindi.
Viongozi wa upinzani wameahidi kushirikiana na kusimamisha mgombea mmoja wa Urais ili kumpinga Rais William Ruto kwenye uchaguzi mkuu ujao.