Rais wa Ufaransa Emmanuel Macron asimamishwa barabarani sababu ya msafara wa Trump

-rickmedia: Saraphina Jerry

Saraphina Jerry

3 days ago
rickmedia: rais-ufaransa-emmanuel-macron-asimamishwa-barabarani-sababu-msafara-trump-315-rickmedia

Rais wa Ufaransa Emmanuel Macron alikumbana na tukio lisilo la kawaida Jumatatu usiku baada ya msafara wake kusimama kwa muda huko Midtown Manhattan, jijini New York, Marekani, wakati wa Mkutano Mkuu wa Umoja wa Mataifa (UNGA).

Macron alikuwa ametoka kutoa hotuba yake katika makao makuu ya UN pindi polisi waliposimamisha msafara wake ili kupisha msafara wa Rais wa Marekani Donald Trump.

Badala ya kusubiri ndani ya gari, Macron alishuka, akampigia Trump simu kwa utani akiomba barabara zifunguliwe, na hatimaye akaamua kutembea kwa miguu.