Vijana wawili waliokanyaga bendera ya Kenya wafikishwa Mahakamani

-rickmedia: Saraphina Jerry

Saraphina Jerry

12 hours ago
rickmedia: vijana-wawili-waliokanyaga-bendera-kenya-wafikishwa-mahakamani-591-rickmedia

Vijana wawili wa Kisomali waliokamatwa wakiwa wanakanyaga bendera ya Kenya katika Uwanja wa Nyayo wakati wa mechi kati ya Mogadishu City Club dhidi ya Kenya Police FC, wamefikishwa mahakamani.

Vijana hao wenye umri wa miaka 14 na 17 wanakabiliwa na mashtaka ya kuharibu alama ya kitaifa ya umoja (bendera ya Kenya), na kusababisha vurugu ikiwa ni kinyume cha sheria.

Hata hivyo, Hakimu Mkazi Rose Gitau ameagiza wapelekwe katika kitengo cha Ulinzi wa Watoto cha Gigiri na kuagiza uchunguzi wa kijamii ufanyike kisha ripoti iwasilishwe mahakamani kabla ya kujibu mashtaka hayo.

Aidha, ndugu wa vijana hao wameomba wawe chini ya ulinzi wao, lakini mahakama imekataa maombi hayo kwa kuwa si wazazi wao wa damu.