Waziri Mkuu wa Israel Benjamin Netanyahu aapa kuiangamiza Hamas

-rickmedia: Saraphina Jerry

Saraphina Jerry

11 hours ago
rickmedia: waziri-mkuu-israel-benjamin-netanyahu-aapa-kuiangamiza-hamas-122-rickmedia

Waziri Mkuu wa Israel Benjamin Netanyahu amehutubia katika Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa na kusisitiza kwamba Israel ni lazima imalize kazi yake iliyoianza ya kulitokomeza kundi la Hamas huko Ukanda wa Gaza.

Kabla Waziri huyo Mkuu kuanza kutoa hotuba, idadi kubwa ya washiriki walitoka nje.

Wakati kiongozi huyo wa Israel akizungumza, kulisikika kelele karibu na eneo la ukumbi. Ujumbe wa Marekani, unaomuunga mkono Netanyahu katika kampeni yake dhidi ya Hamas ulikuwa umetulia tuli. Na kwa upande mwingine kulisikika makofi mara tu alipoanza kuhutubia.

Mataifa machache makubwa yaliyohudhuria kama Marekani na Uingereza hayakupeleka maafisa wake waandamizi ama mabalozi wao wakati wa hotuba hii na badala yake viti vyao vilijaa maafisa na wanadiplomasia wa ngazi za chini.

"Viongozi wa magharibi wanaweza kukubaliana na mashinikizo, lakini ninawahakikishia kitu kimoja, Israel kamwe haitabadilika." amesema Netanyahu

Ametumia jukwaa hilo kuyakosoa vikali mataifa ya magharibi kwa kulikumbatia suala la utaifa wa Palestina na kuyatuhumu kwa kubadilika ghafla kufuatia mashinikizo kutoka kwa wanaharakati na wengine wanaoishutumu Israel kwa uhalifu wa kivita dhidi ya Wapalestina huko Gaza.

Ikumbukwe kuwa Mahakama ya Kimataifa ya Uhalifu - ICC tayari imetoa waranti wa kukamatwa Netenyahu kwa madai ya uhalifu wa kivita huko Gaza.