Mkutano Wa Rais Donald Trump Na Rais Vladmir Putin wasitishwa kwa muda

-rickmedia: Saraphina Jerry

Saraphina Jerry

10 hours ago
rickmedia: mkutano-rais-donald-trump-rais-vladmir-putin-wasitishwa-kwa-muda-540-rickmedia

Mkutano uliopangwa kufanyika Budapest kati ya Rais wa Marekani Donald Trump na Rais wa Urusi Vladimir Putin umesitishwa baada ya Urusi kukataa pendekezo la kusitisha mapigano nchini Ukraine.

Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani, Marco Rubio, ametangaza kusitishwa kwa mkutano huo baada ya mazungumzo na mwenzake wa Urusi, Sergei Lavrov. Trump amethibitisha hatua hiyo, akisema hataki mkutano usio na tija.

Hata hivyo, Urusi imesema maandalizi yanaendelea, lakini masuala muhimu lazima yakubaliwe kwanza.