Ndege ya mizigo yaanguka baharini HongKong, yaua watu wawili

-rickmedia: Saraphina Jerry

Saraphina Jerry

11 hours ago
rickmedia: ndege-mizigo-yaanguka-baharini-hongkong-yaua-watu-wawili-680-rickmedia

Ndege ya mizigo ya Shirika la Ndege la Emirates, imeanguka baharini leo Jumatatu, Oktoba 20, 2025, muda mfupi baada ya kuanza kuruka katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Hong Kong, nchini China.

Taarifa za awali zinaeleza ajali hiyo imetokea baada ya ndege hiyo aina ya Boeing 747-481 kugonga gari la doria lililokuwa kwenye eneo la kurukia ndege, na kusababisha vifo vya watu wawili waliokuwa ndani ya gari hilo.

Mashuhuda waliokuwa eneo la tukio wamesema ndege hiyo ilivunjika vipande viwili kabla ya kuelea baharini, huku wafanyakazi wanne waliokuwa ndani ya ndege wakinusurika kifo na kupata majeraha madogo.

Ajali hiyo imetajwa kuwa ni tukio la pili kuhusisha vifo katika uwanja wa ndege wa sasa wa Hong Kong tangu ulipoanza kutumika mwaka 1998, na mamlaka za anga zimeanzisha uchunguzi kubaini chanzo chake.