Rapa Lil Durk, ambaye ametimiza miaka 33 Oktoba 19, ametuma ujumbe maalum siku ya kuzaliwa kwake akiwa gerezani.
Kupitia mawasiliano ya simu, Durk alisema, “Niko vizuri zaidi. Kila mtu anapewa nafasi ya pili… nikitoka hapa, nitaongoza kwa mfano.” Amedai kuwa amejifunza mengi na anataka kuonyesha mabadiliko yake kwa vitendo, si kwa maneno.
Durk alikamatwa Oktoba 2024 huko Broward, Florida, kwa tuhuma za mauaji ya kulipia (murder for hire) yanayohusiana na kifo cha Saviay’a “Lul Pab” Robinson, binamu wa rapper Quando Rondo.
Shambulio hilo la mwaka 2022 lilidaiwa kuwa ni kulipiza kisasi kwa kifo cha King Von (2020). Kwa sasa anashikiliwa bila dhamana, akikabiliwa na mashtaka ya njama ya mauaji, matumizi ya silaha bila kibali, na mauaji ya kulipia.