Raila Odinga Afariki Dunia akipatiwa matibabu nchini India

-rickmedia: Saraphina Jerry

Saraphina Jerry

6 hours ago
rickmedia: raila-odinga-afariki-dunia-akipatiwa-matibabu-nchini-india-939-rickmedia

Aliyekuwa Waziri Mkuu wa Kenya, Raila Odinga amefariki dunia akiwa nchini India alikokuwa akipatiwa matibabu.

Kwa mujibu wa Nation Media, taarifa za kifo cha Raila (80), ambaye pia ni Kiongozi wa Chama cha Orange Democratic Movement (ODM), zimethibitishwa na mmoja wa wasaidizi wa ofisi yake.

Raila alihudumu kama Waziri Mkuu wa Kenya katika kipindi 2008–2013 na alijulikana kwa msimamo wake wa kutetea demokrasia na haki za binadamu.