Metro Boomin Ashinda Kesi ya Madai ya Unyanyasaji wa Kingono; Mahakama Yamkuta Hana Hatia

-rickmedia: Lanka Ting

Lanka Ting

1 day ago
rickmedia: metro-boomin-ashinda-kesi-madai-unyanyasaji-kingono-mahakama-yamkuta-hana-hatia-875-rickmedia

Msanii na mtayarishaji maarufu wa muziki, Metro Boomin, ameshinda kesi ya madai ya unyanyasaji wa kingono iliyokuwa imefunguliwa dhidi yake na Vanessa LeMaistre, aliyedai kutendewa ukatili wa kingono mwaka 2016 baada ya kuleweshwa kwa kutumia pombe na dawa.

Baada ya kusikiliza ushahidi na hoja kutoka pande zote kwa muda wa siku tatu, jopo la majaji limeamua kuwa Metro Boomin hana hatia kuhusiana na madai hayo.

LeMaistre alikuwa anadai fidia ya zaidi ya dola milioni 3, akisisitiza kuwa tukio hilo lilitokea bila ridhaa yake. Hata hivyo, Metro Boomin kupitia mawakili wake, alikana vikali tuhuma hizo, akieleza kuwa uhusiano wao ulikuwa wa hiari na kwamba madai hayo ni sehemu ya njama ya kumtapeli kifedha.

Aidha, Metro alikanusha madai kuwa alijigamba kuhusu tukio hilo katika wimbo Rap Saved Me uliotolewa mwaka 2017, akisisitiza kuwa kazi yake ya muziki haipaswi kufasiriwa kama ushahidi wa vitendo vya kihalifu.

Kwa sasa, Metro Boomin ameahidi kuendelea na kazi zake za muziki na kushukuru mashabiki wake kwa uungwaji mkono alioupokea wakati wa kipindi hiki kigumu.