Mjane Alice Haule Atuma Maombi Asiondolewe kwenye Nyumba

-rickmedia: Lanka Ting

Lanka Ting

1 day ago
rickmedia: mjane-alice-haule-atuma-maombi-asiondolewe-kwenye-nyumba-611-rickmedia

Mjane wa marehemu Justice Rugaibula, Alice Hause, amewasilisha maombi madogo Na.24541/2025 katika Mahakama Kuu Divisheni ya Ardhi, akiomba zuio la muda kuondolewa kwenye nyumba yake iliyopo Msasani Beach, Kiwanja Na.819, Hati Na.49298.

Kwa mujibu wa taarifa ya Mahakama iliyotolewa na Gerard Julius Chami, shauri hilo na jingine alilofungua Alice yako katika hatua mbalimbali.

Awali, maombi yake ya madai ya ardhi yalikataliwa Septemba 19, 2025 kwa mapungufu ya kisheria, lakini baada ya marekebisho, Septemba 24, 2025 shauri hilo limesajiliwa upya kwa Na.24396/2025 likiwa na marekebisho ya kumuongeza Msajili wa Hati kama mdaiwa.