NASA imethibitisha uwepo wa mwezi mdogo wa muda mfupi unaozunguka Dunia, tukio la nadra ambalo litaendelea hadi mwaka 2083. Mwezi huu mdogo, unaojulikana kama 2024RM, umevutwa na mvuto wa Dunia na kwa sasa unasafiri sambamba na sayari yetu.
Wanasayansi wanasema kuwa kipande hiki ni satelaiti ya asili chenye ukubwa wa gari dogo, ambacho huenda ni asteroidi iliyokamatwa na mvuto wa Dunia. Hii inaiunganisha na Mwezi mkuu katika kile wanasayansi wanachokiita “quasi-satellite”.
Ingawa hakina hatari yoyote kwa Dunia, watafiti wana hamu ya kuchunguza mwelekeo wake, muundo, na tabia yake katika miaka ijayo.
Hii ni fursa adimu kwa wanaanga kuchunguza satelaiti asilia inayozunguka Dunia, ikitoa mwanga mpya na mwenendo wa asteroid ndogo zinazoweza kuingia kwenye mfumo wa jua.