Mbunge wa jimbo la Ilala Mheshimiwa Mussa Hassan Zungu ambaye alikuwa akiwania nafasi ya Spika wa Bunge ameshinda nafasi hiyo na kuwa Spika wa Bunge la Jamuhuri Ya Muungano Wa Tanzania.
Zungu ameshinda nafasi hiyo kwa kuchaguliwa na Wabunge wenza wa Bunge la Jamuhuri Ya Muungano Wa Tanzania katika uchaguzi uliofanyika leo Novemba 11, 2025, mjini Dodoma.
Jumla ya kura 383 zilipigwa, 3 zikiharibika. Zungu alipata kura 378, Anita kura 1, huku Voinca Charles, Nyakitita, na Amini hawakupata kura yoyote.
Ikumbukwe Zungu alikuwa kwenye nafasi ya Naibu Spika wa Bunge la Jamuhuri Ya Muungano Wa Tanzania tangu mwaka 2022 mpaka mwaka 2025 kipindi ambacho Spika wa Bunge alikuwa Dkt.Tulia Ackson hivyo kiti hicho sio kigeni kwake kwani ana uzoefu na kazi zake
Hongera sana kwa Mheshimiwa Mussa Hassan Zungu