Rapa Lil Uzi Vert ashtakiwa kwa kosa la unyanyasaji

-rickmedia: Saraphina Jerry

Saraphina Jerry

2 days ago
rickmedia: rapa-lil-uzi-vert-ashtakiwa-kwa-kosa-unyanyasaji-94-rickmedia

Rapa wa Marekani Lil Uzi Vert ameripotiwa kushitakiwa na aliyekuwa msaidizi wake binafsi, mwanamke anayemdai alimnyanyasa alipokuwa akifanya kazi naye mwaka 2022.

Msaidizi huyo anadai alipata msongo wa mawazo, unyanyasaji wa kihisia, kimwili na wa kingono wakati wa kazi, hasa alipokuwa akiongozana na Uzi kwenye ziara zake. Pia anasema baadhi ya wanachama wa Roc Nation, timu ya usimamizi wa Uzi, walihusika au walifumbia macho tabia hiyo.

Kwa sasa, mwanamke huyo amefungua kesi mahakamani akitaka fidia na haki kutokana na madai hayo ya unyanyasaji.