Elipidius Balthazar, mkazi wa Wilaya ya Muleba mkoani Kagera, amehukumiwa kifungo cha maisha jela kwa kosa la kubaka.
Inadaiwa mshtakiwa alitenda kosa hilo tarehe 19 Septemba 2025 katika Kijiji cha Kabirizi, Wilaya ya Muleba, Mkoa wa Kagera.
Baada ya tukio hilo, alikamatwa na Jeshi la Polisi na kufikishwa mahakamani tarehe 1 Oktoba 2025. Hukumu hiyo imetolewa tarehe 10 Novemba 2025 na Mhe. Lilian Mwambeleko, Hakimu wa Mahakama ya Wilaya ya Muleba.