Nicolas Sarkozy aachiwa baada ya kushikiliwa kwa wiki 3

-rickmedia: Saraphina Jerry

Saraphina Jerry

1 day ago
rickmedia: nicolas-sarkozy-aachiwa-baada-kushikiliwa-kwa-wiki-367-rickmedia

Rais wa zamani wa Ufaransa, Nicolas Sarkozy, ameachiliwa wiki tatu baada ya kuanza kutumikia kifungo cha miaka mitano kwa kosa la kula njama ya kufadhili kampeni yake ya urais ya 2007 kwa pesa kutoka kwa aliyekuwa kiongozi wa Libya, Muammar Gaddafi.

Sarkozy, mwenye umri wa miaka 70, ataendelea kuwa chini ya uangalizi mkali wa mahakama na amezuiwa kuondoka Ufaransa. Mawakili wake wamewasilisha ombi la rufaa, ambalo litaskilizwa mwezi Machi mwaka ujao.