Kesi ya uhaini inayomkabili Mwenyekiti wa CHADEMA Taifa, Tundu Lissu, iliyokuwa iendelee leo Jumatatu, Novemba 10, 2025, imeahirishwa hadi Jumatano, Novemba 12, 2025.
Mahakama imeahirisha kesi hiyo baada ya upande wa Jamhuri kushindwa kumleta shahidi wa nne kutoka mikoa ya Ruvuma na Mbeya kutokana na hali ya usalama kutokuwa thabiti jijini Dar es Salaam.
Wakili wa Serikali Mkuu, Thawabu Issa, aliomba kesi iahirishwe chini ya kifungu cha 302(a) cha Sheria ya Mwenendo wa Makosa ya Jinai (Sura ya 20, Toleo la 2023) kwa muda wa siku 14, lakini Jaji Danstan Ndunguru alikubali kuahirisha hadi Novemba 12, 2025 pekee.