Kesi ya mauaji Rapa #YNWMelly imeahirishwa hadi mwaka 2027.
Takribani miaka minane tangu kukamatwa kwake mwaka 2019, #YNWMelly ataendelea kusalia gerezani akisubiri kesi inayomkabili ya tuhuma za kumuua #YNWSakchaser na #YNWJuvy mwaka 2018.
Kesi hiyo, ambayo awali ilipangwa kuanza Septemba 10, imeahirishwa baada ya pande zote mbili kukata rufaa kuhusu ushahidi gani unaweza kutumika, na mahakama ya rufaa ya Florida kuamuru kusitishwa kwa mchakato wote hadi suala hilo litakapotatuliwa.
Kesi yake ya kwanza mwaka 2023 ilimalizika bila uamuzi baada ya majaji kushindwa kukubaliana. Mshitakiwa mwenza, YNW Bortlen, anakabiliwa na kesi tofauti.