Serikali yatangaza ajira za wahudumu wa afya 8,900

-rickmedia: Saraphina Jerry

Saraphina Jerry

1 year ago
rickmedia: serikali-yatangaza-ajira-wahudumu-afya-8900-994-rickmedia

Serikali imetangaza nafasi za kazi kwa wahudumu wa afya ngazi ya jamii 8,900 watakaokwenda kutekeleza afua jumuishi za afya, lishe na ustawi wa jamii katika ngazi ya vitongoji na vijiji.

Tangazo limelotolewa leo Jumamosi Aprili 6, 2024 na Wizara ya Afya kwa ushirikiano na Ofisi ya Rais Tamisemi likieleza kuwa, hivi sasa Serikali inatekeleza mpango jumuishi wa wahudumu wa afya wa ngazi ya jamii nchini.

Kupitia mpango huo, Serikali imeweka utaratibu wa kuwapata wahudumu wenye sifa zilizowekwa kutoa mafunzo na kuwatumia wahudumu wa afya ngazi ya jamii katika utekelezaji wa afua hizo.

Kwa mujibu wa tangazo hilo, awamu ya kwanza ya mpango huo utaanza kwenye mikoa 10 na halmashauri mbili kwa kila mkoa.

Mikoa itakayonufaika ni Geita wahudumu 920, Kagera (878), Kigoma (1094), Lindi (1724), Mbeya (836), Njombe (746), Pwani (480), Songwe (774), Tabora (966) na Tanga (482).