Loading...

Watu takribani 15O wamefariki dunia kutokana na mlipuko wa kipindupundi uliotokea Harare nchini Zimbawe.

-rickmedia: Saraphina Jerry

Saraphina Jerry

6 months ago
rickmedia: watu-takribani-15o-wamefariki-dunia-kutokana-mlipuko-kipindupundi-uliotokea-harare-nchini-zimbawe-610-rickmedia

Taarifa iliyotolewa Jumatatu Novemba 20, 2023 na Wizara ya Afya nchini humo, imetangaza ugonjwa huo kuwa janga la taifa na kuutangaza mjini wa Harare kuwa katika hali ya hatari zaidi.

Ijumaa mwishoni mwa wiki iliyopita Wizara ya Afya nchini humo, ilitangaza Jiji la Harare lenye wakazi zaidi ya milioni 1.5 kuwa ndiyo mji ulioathirika , huku zaidi ya watu 7,000 wakiwa katika uangalizi maalumu.

Waziri wa Afya, Dk Douglas Mombeshara amesema nusu ya vifo vilivyotokea ni kutoka eneo la Kuwadzana.

Imeelezwa kwamba mlipuko wa kipindupndu umekuwa ukitokea mara kwa mara katika mji huo kutokana na miundombinu mibovu usambazaji majisafi iliyokuwapo kwa muda mrefu.

“Watu wanakunywa maji ambayo ni ya visima, yasiyotembea hii inamaanisha kwamba maji hayo yanakuwa yameathiriwa na vijidudu: amesema Meya wa Jiji la Harare, Ian Makone.