WHO:Maambikizi ya magonjwa ya zinaa hasa Kaswende kwa wenye miaka 15-49 yameongezeka

-rickmedia: Saraphina Jerry

Saraphina Jerry

1 year ago
rickmedia: whomaambikizi-magonjwa-zinaa-hasa-kaswende-kwa-wenye-miaka-15-49-yameongezeka-125-rickmedia

Kwa mujibu wa Ripoti mpya iliyotolewa na Shirika la Afya Duniani (WHO) inaeleza Watu zaidi ya milioni 1 (Miaka 15-49) huambukizwa Magonjwa ya Zinaa ikiwemo Kaswende na Kisonono huku Maambukizi mengi yakitokea Barani Amerika na Afrika.

Takwimu mpya zinaonesha Magonjwa ya Zinaa yanaongezeka katika maeneo mengi. Mnamo 2022, Nchi Wanachama wa WHO ziliweka lengo la kupunguza idadi ya kila Mwaka ya Maambukizi ya Kaswende kwa Watu wazima mara kumi ifikapo 2030, kutoka milioni 7.1 hadi 710,000.

Hata hivyo, visa vipya vya Kaswende miongoni mwa Watu wazima wenye umri wa Miaka 15-49 viliongezeka kwa zaidi ya milioni 1 Mwaka 2022 na kufikia milioni 8. Ongezeko la juu zaidi lilitokea katika Kanda ya Amerika na ya Afrika.