Australia yapiga marufuku watoto chini ya miaka 16 kutumia mitandao ya kijamii, kuanzia Disemba 10,2025

-rickmedia: Saraphina Jerry

Saraphina Jerry

2 days ago
rickmedia: australia-yapiga-marufuku-watoto-chini-miaka-kutumia-mitandao-kijamii-kuanzia-disemba-102025-153-rickmedia

Australia imepitisha marufuku ya kihistoria inayozuia watoto walio chini ya miaka 16 kutumia mitandao ya kijamii kuanzia Desemba 10, 2025. Kampuni za mitandao kama Facebook, Instagram, TikTok, X na nyingine zitapaswa kuthibitisha umri wa watumiaji kupitia teknolojia kama utambuzi wa sura, sauti au vitambulisho vya serikali. Akaunti za watoto chini ya umri huo zitafutwa au kuzimwa.

Serikali inasema hatua hiyo inalenga kupunguza madhara ya maudhui hatarishi na utegemezi wa skrini, baada ya utafiti kuonyesha asilimia 96 ya watoto wa miaka 10–15 hutumia mitandao hiyo na wengi hukutana na maudhui yenye vurugu, chuki au hatari kwa afya ya akili.

Wakosoaji wanaonya kuhusu hatari za uvunjifu wa faragha na uwezekano wa vijana kukwepa sheria kwa kutumia VPN au taarifa za umri za uongo. Hii ni sera ya kwanza duniani ya kiwango hiki, na mataifa mengine yanaiangalia kwa makini.