Rais amteua Lazaro Nyalandu kuwa mshauri wake wa Kidiplomasia

-rickmedia: Saraphina Jerry

Saraphina Jerry

4 days ago
rickmedia: rais-amteua-lazaro-nyalandu-kuwa-mshauri-wake-kidiplomasia-251-rickmedia

Rais Samia Suluhu Hassan amemteua Balozi Lazaro Nyalandu kuwa Mshauri wa Rais katika masuala ya Diplomasia.

Taarifa ya uteuzi huo imetolewa Novemba 21, 2025 na Katibu Mkuu Kiongozi Balozi Dk Moses Kusiluka na kusainiwa na Mkurugenzi wa Mawasiliano Ikulu, Bakari Machumu.

Uteuzi huo wa Nyalandu unakuja siku chache baada ya Rais Samia Suluhu Hassan kumteua kuwa Balozi.

Nyalandu amewahi kuhudumu katika nafasi mbalimbali za uongozi ikiwemo Mbunge wa Singida Kaskazini.

Pia nafasi ya uwaziri katika Serikali ya awamu ya nne iliyokuwa ikiongozwa na Rais mstaafu Jakaya Kikwete na wizara ya mwisho kuhudumu ilikuwa ya Maliasili na Utalii.

Vilevile amewahi kuwa mmoja wa washauri wa aliyekuwa Mke wa Rais wa Awamu ya Tatu, Mama Anna Mkapa katika uendeshaji wa Mfuko wa Fursa Sawa kwa Wote (EOTF).