Mahakama ya Wilaya ya Ilemela jijini Mwanza imewaachia huru watuhumiwa 57 wa kesi ya uhaini waliokamatwa baada ya vurugu za uchaguzi.
Hatua hiyo imekuja baada ya upande wa mashtaka kuwasilisha ombi la DPP kutokuwepo na nia ya kuendelea na mashtaka.
Hakimu Mkazi Mkuu Stella Kiama ametangaza kufutwa kwa mashtaka hayo leo, wakati shauri hilo namba 26641/2025 likiletwa kwa ajili ya kutajwa kwa mara ya pili. Watuhumiwa 4 pekee kati ya 61 bado wanaendelea na mchakato wa mashtaka.