Christian Ronaldo akutana na Rais wa Marekani Donald Trump

-rickmedia: Saraphina Jerry

Saraphina Jerry

8 hours ago
rickmedia: christian-ronaldo-akutana-rais-marekani-donald-trump-139-rickmedia

Cristiano Ronaldo ameshea picha inayoonyesha akipeana mkono na Rais wa Marekani, Donald Trump, ndani ya Ofisi ya Oval. Kupitia ujumbe mfupi aliouandika, Ronaldo alimshukuru Trump kwa mwaliko na mapokezi aliyoyapata yeye pamoja na mchumba wake, Georgina Rodriguez.

Ronaldo alieleza kuwa kila mtu ana mchango muhimu katika jamii, akisisitiza dhamira yake ya kuendelea kuwa mfano kwa vizazi vipya kupitia maadili ya ujasiri, uwajibikaji na amani ya kudumu. Ujumbe wake umeibua mazungumzo makubwa, hasa kutokana na ushawishi wake mkubwa duniani na nafasi ya tukio hilo kisiasa na kijamii.

Hata hivyo, kitendo hicho kimetafsiriwa pia kama ishara ya ushawishi wake nje ya ulingo wa michezo, kikiwaonyesha mashabiki namna ambavyo Ronaldo anajikita katika masuala mapana zaidi ya soka.