Watumiaji wa Twitter/X kujulikana mahali walipo

-rickmedia: Saraphina Jerry

Saraphina Jerry

1 day ago
rickmedia: watumiaji-twitterx-kujulikana-mahali-walipo-226-rickmedia

Katika kudhibiti matumizi ya akaunti feki pamoja na wale wanaotoa taarifa za uongo mtandao wa X (zamani Twitter), umekuja na kipengele kipya kitakachoonyesha mahali alipo mtumiaji wa akaunti husika.

Kupitia kipengele hicho cha ‘About this Account’ inatonesha nchi ambayo akaunti imefunguliwa, mtumiaji amebadili jina la akaunti mara ngapi, mtumiaji anatumia akaunti husika kupitia simu ya Android au Iphone.

Kwa mujibu wa kampuni hiyo, lengo ni moja: kuwapa watumiaji muktadha wa kutosha ili kutambua kama akaunti ni ya kweli au inajaribu kusambaza taarifa potofu. Kwa mfano, akaunti inayodai kuwa Marekani lakini taarifa zinaonyesha imekuwa ikitumia mtandao kutoka nchi nyingine inaweza kuzua maswali juu ya uhalisia wake.

Taarifa hizo sasa zinapatikana juu ya ukurasa wa wasifu (profile), chini ya jina la mtumiaji. Ukibonyeza sehemu ya “Joined,” utapelekwa kwenye ukurasa unaoitwa About this account.

Kupitia taarifa iliyochapishwa kwenye The New York Times, BBC na mitandao ya teknolojia kipengele hicho, kimetangazwa mwishoni mwa wiki na Mkuu wa Bidhaa wa X, Nikita Bier.