Jeshi la Israeli limetangaza kukamilisha mashambulizi dhidi ya maeneo ya kijeshi ya Hezbollah kusini mwa Lebanon, likidai yalilenga maghala ya silaha ya kikosi cha Radwan ambacho kinadaiwa kujipanga upya kinyume na makubaliano ya kusitisha mapigano.
Kabla ya operesheni hiyo, IDF iliwaonya wakazi kuondoka katika maeneo maalum katika kusini mwa Lebanon. Walinda amani wa Umoja wa Mataifa wamelaani mfululizo wa mashambulizi hayo, huku Rais wa Lebanon, Joseph Aoun, akiyataja kama uhalifu mkubwa unaofanywa na Israeli.