Mama wa mfanyabiashara Niffer amuombea msamaha binti yake kwa Rais Samia

-rickmedia: Saraphina Jerry

Saraphina Jerry

6 hours ago
rickmedia: mama-mfanyabiashara-niffer-amuombea-msamaha-binti-yake-kwa-rais-samia-200-rickmedia

Mama mzazi wa Mfanyabiashara Jeniffer Jovin maarufu kama Niffer amejitokeza na kumuombea Binti yake Msamaha kwa Mheshimiwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt Samia Suluhu Hassan huku akisisitiza kuwa yeye hana msaada zaidi ya binti yake huyo kwani hana kazi yoyote anayofanya yeye ni mgonjwa.

Mfanyabiashara Niffer alikamatwa na Polisi Oktoba 27.2025 kwa madai ya Kuhamasisha Vurugu, taarifa iliyotolewa na wakili Peter Kibatala hivi karibuni ni kuwa Niffer yuko salama na jopo la mawakili linaendelea kushughulikia kesi yake hiyo.