Alikiba awaomba msamaha wananchi wa Tanzania kwa kilichotokea

-rickmedia: Saraphina Jerry

Saraphina Jerry

2 hours ago
rickmedia: alikiba-awaomba-msamaha-wananchi-tanzania-kwa-kilichotokea-665-rickmedia

Msanii na mfalme wa muziki wa Bongoflava Ally Kiba amerudi kwa wananchi wa Tanzania kuwaomba radhi kwa kukaa kimya kwa kipindi ambacho kulikuwa na machafuko nchini.

Ikumbukwe kwenye uchaguzi mkuu wa Tanzania kulitokea machafuko ambayo yalisababisha vifo vingi vya wanachi na wananchi walichukizwa na ukimya wa wasanii (Vioo vya jamii) kukaa kimya kwenye hilo bila kukemea chochote.

Alikiba anaungana na wasanii wengine waliotoa neno baada ya machafuko haya baadhi yao ikiwa ni Diamond Platnumz,Zuchu,Nandy,Rayvanny,T.I.D na wengine wengi.