Rapa Chemical aomba wananchi wasiwasamehe kwa kutokuwa upande wao kipindi kigumu

-rickmedia: Saraphina Jerry

Saraphina Jerry

2 hours ago
rickmedia: rapa-chemical-aomba-wananchi-wasiwasamehe-kwa-kutokuwa-upande-wao-kipindi-kigumu-128-rickmedia

Rapa Chemical ameungana na watanzania wengi ambao wameshangazwa na namna ambavyo watu maarufu hasa wasanii walivyokaa kimya wakati nchi ilikuwa ikipitia kipindi kigumu huku akisisitiza kuwa kwa hilo wamekosea sana na wasisamehewe.

Ukiachana na Chemical msanii mwingine aliyekiri makosa yao wasanii ya kujitenga na wananchi kipindi ambacho waliwahitaji zaidi ni Kussah, wasanii wote hawa wanayaona makosa yao ya wazi na hawaoni kama wao kama wasanii wanastahili kusamehewa.

Suala la wasanii kukaa kimya kwenye jambo hili limekuwa mjadala mkubwa mtandaoni mpaka baadhi ya wananchi wameanzisha kampeni za kuacha kuwafuata wasanii kwenye mitandao (Kuwa-Unfollow) ili kuwaonyesha kuwa wamechukizwa na jambo walilolifanya.