Binti afahamikae kwa jina la Emman Atienza anayejulikana kwa video zake maarufu za mtindo wa maisha kwenye TikTok amefariki dunia nyumbani kwake jijini Los Angeles siku ya Jumatano … TMZ imeripoti
Kwa mujibu wa Ofisi ya Mpelelezi wa Vifo wa Kaunti ya Los Angeles, chanzo cha kifo cha Atienza kimetajwa kuwa ni kujiua, kifo chake kimeleta simazi kubwa mitandaoni pamoja na familia yake.
Emman alikuwa na zaidi ya wafuasi Laki Nane ( 800,000 ) kwenye TikTok na Laki Mbili Na Elfu 25 (225,000) kwenye Instagram. Video zake za karibuni zaidi zilihusu maisha yake mapya huko Los Angeles, ambako alihamia majira ya kiangazi yaliyopita.