Mahakama yatupa shauri la Polepole, yataja sababu

-rickmedia: Saraphina Jerry

Saraphina Jerry

3 hours ago
rickmedia: mahakama-yatupa-shauri-polepole-yataja-sababu-164-rickmedia

Mahakama Kuu Masjala Ndogo Dar es Salaam imetupilia mbali shauri la maombi ya amri ya kumfikisha mahakamani au kumwachia kwa dhamana (Habeas corpus), Humphrey Polepole, ikieleza hakuna ushahidi kuwa wajibu maombi ndio waliomchukua.

Uamuzi huo ulioandikwa na Jaji Mfawidhi wa Mahakama hiyo, Salma Maghimbi, aliyesikiliza shauri hilo umesomwa leo Oktoba 24, 2025 na Naibu Msajili wa mahakama hiyo, Livin Lyakinana.