Huduma za Internet zazorota Cameroon matokeo ya Urais yakisubiriwa

-rickmedia: Saraphina Jerry

Saraphina Jerry

3 hours ago
rickmedia: huduma-internet-zazorota-cameroon-matokeo-urais-yakisubiriwa-932-rickmedia

Upatikanaji wa huduma za intaneti nchini Cameroon umedhoofika kwa kiasi kikubwa huku maandamano yakiendelea kufuatia madai ya udanganyifu katika uchaguzi wa urais uliofanyika Oktoba 12, mwaka huu.

Taasisi ya kufuatilia huduma za mtandao duniani, NetBlocks, imethibitisha hilo jana, Alhamisi Oktoba 23, 3035 kuwa kumekuwa na usumbufu unaoendelea wa intaneti nchini humo, hali inayoweza kuathiri ufuatiliaji na uandishi wa habari kuhusu matukio yanayoendelea.

Hayo yanajiri siku moja baada ya Baraza la Katiba nchini humo kutupilia mbali rufaa zote zilizokuwa zikilalamikia matokeo ya uchaguzi huo, hatua inayofungua njia kwa tume ya uchaguzi kutangaza matokeo kamili.