Rapa Kanye West ambaye ni baba Mzazi wa Mwanae North West amechukizwa vikali kwa matumizi mabaya ya mitandao ya kijamii anayofanya binti yake kwa kutumia Tiktok na kuposti video akiwa na muonekano wa Tattoo usoni na nywele zenye rangi ya blue.
Binti huyo wa Kim Kardashian pamoja na Kanye West, North west mwenye umri wa miaka 12 ameteka vichwa vya habari mitandaoni baada ya kuposti video akionekana na Tattoo feki usoni, nywele zenye rangi ya blue, lensi za macho ya blue na kupaka hina kwenye mikono yake, video iliyotembea sana mitandaoni.
Kitendo hicho kimempa wasiwasi Kanye na akidai kuwa Kim Kardashian anahusika katika kumuhimiza binti yao kufanya vitendo ivyo na kupelekea kukua kwa haraka Sana.