Msanii kutoka nchini Nigeria Yemi Alade, amesimulia namna alivyowahi, alijipunguzia miaka mitatu kutoka kwenye umri wake wa kweli. Yemi anasema wakati huo alikuwa na miaka 25 kiuhalisia lakini alikuwa akidai kuwa ana miaka 22.
Yemi amesema kitendo hicho kilimfanya apate msongo wa mawazo (Depression) kutokana na ugumu wa kuishi na uongo huo na kutokukubali ukweli kuhusu umri wake halisi.
Yemi Alade sio msanii wa kwanza kudanganya kuhusu umri wake ni wasanii wengi sana hufanya hivyo na wengi wao huwa hawajitokezi kusema ukweli kama alivyofanya Yemi. Wasanii wamekuwa wakidanganya kuhusu umri wao ili waonekane wadogo mpaka imegeuka kama utamaduni kwa mastaa wengi hasa kwa hapa Tanzania.
Je ni msanii gani unamkubuka ambaye aliwahi kujichanganya kwa kutaja umri wake kwa kudanganya?