Talaka ya Kanye West na Kim Kardashian ilimsababishia Kim Uvimbe kwenye Ubongo

-rickmedia: Saraphina Jerry

Saraphina Jerry

5 hours ago
rickmedia: talaka-kanye-west-kim-kardashian-ilimsababishia-kim-uvimbe-kwenye-ubongo-362-rickmedia

Kwenye kipande cha utangulizi wa msimu wa 7 wa kipindi cha The Kardashians kinachoonyeshwa kupitia Hulu, Kim Kardashian amefichua kuwa madaktari waligundua uvimbe wa damu kwenye ubongo baada ya kufanyiwa uchunguzi wa MRI.

Kim alionekana akiambia familia yake, “Kulikuwa na uvimbe mdogo wa damu,” na kuongeza kuwa madaktari wamehusisha hali hiyo na msongo wa mawazo, hasa kutokana na changamoto alizopitia kufuatia talaka yake na Ye (Kanye West).

Kwa mujibu wa Mayo Clinic, uvimbe wa damu kwenye ubongo ni hali ambapo mshipa wa damu unapungua nguvu na kuvimba, hali ambayo inaweza kusababisha damu kuvuja kwenye ubongo endapo utapasuka.