Shirika la Afya Duniani (WHO) limesema kuwa huduma za matibabu bado hazijarejea kikamilifu kwa wakazi wa Ukanda wa Gaza, takriban wiki mbili tangu kuanza kwa makubaliano ya kusitisha mapigano.
Akiwa mjini Geneva, mwakilishi wa WHO katika maeneo yanayokaliwa na Israel, Rik Peeperkorn, amesema usambazaji wa dawa na vifaa vya matibabu vilivyokuwa vimezuiwa kwa miezi kadhaa, umeanza kufikishwa katika baadhi ya maeneo ya Gaza.
Peeperkorn amesema ukweli kwamba Israel imefungua vivuko viwili pekee vya mpaka unafanya iwe vigumu kukidhi mahitaji makubwa ya kiafya ya eneo hilo.