Asap Rocky na Rihanna hawajaajiri mfanyakazi wanalea watoto wao wenyewe

-rickmedia: Saraphina Jerry

Saraphina Jerry

3 hours ago
rickmedia: asap-rocky-rihanna-hawajaajiri-mfanyakazi-wanalea-watoto-wao-wenyewe-394-rickmedia

Rapa Asap Rock na mama watoto wake Rihanna hawajaajiri mfanyakazi yeyote kwaajili ya kuwasaidia kwenye malezi ya watoto zao bali wao wenyewe binafsi wanafanya kazi hiyo kwani wanahitaji zaidi kuwa karibu na watoto wao hao katika makuzi yao.

Asap na Rihanna hawakuajiri Msaidizi wa kazi baada ya kuzaliwa kwa mtoto wao wa kwanza, RZA Athelston Mayers, waliamua kumtunza wao wenyewe, baadaye walipokea watoto wengine wawili, Riot Rose Mayers, na binti yao Rocki Irish Mayers na mpaka sasa hawajatafuta msaidizi wa kuwasaidia kuwatunza watoto wao bali wanafanya wenyewe kazi hiyo bado.

Kwenye moja kati ya mahojiano aliyowahi kuyafanya Rihanna alisema asingeweza kuajiri msaidizi kwani yeye hakusubiri miaka 35 apate mtoto ili mtu mwingine aje amsaidie kulea.