Tajiri Aliko Dangote aweka rekodi mpya Afrika

-rickmedia: Saraphina Jerry

Saraphina Jerry

2 hours ago
rickmedia: tajiri-aliko-dangote-aweka-rekodi-mpya-afrika-229-rickmedia

Ripoti kutoka Mabilionea Bloomberg Mfanyabiashara mkubwa wa nchini Nigeria, Aliko Dangote, ameandika historia mpya kwa kuwa Mwafrika wa kwanza kufikisha utajiri wa Dola Bilioni 30.3.

​Utajiri huu wa Dangote, ambao umeongezeka kwa Dola Bilioni 2.25 mwaka huu, unachangiwa pakubwa na biashara zake za saruji, mafuta, na mbolea.

Moja ya miradi yake mikubwa inayochangia utajiri huu ni kiwanda cha saruji chenye thamani ya Dola Milioni 160 nchini Côte d'Ivoire, pamoja na kiwanda chake kikubwa cha kusafisha mafuta cha Nigeria, kinachokadiriwa kuwa na thamani ya Dola Bilioni 20.