Elizabeth Michael "Lulu" aililia amani ya Tanzania "Tusamehe kwa kuchukulia kawaida uliyotupa"

-rickmedia: Saraphina Jerry

Saraphina Jerry

2 hours ago
rickmedia: elizabeth-michael-lulu-aililia-amani-tanzania-tusamehe-kwa-kuchukulia-kawaida-uliyotupa-166-rickmedia

Mwigizaji kutoka nchini Tanzania Eizabeth Michael maarufu kama "Lulu" ameungana na mamia ya watanzania walioonyesha maumivu yao kupitia mitandao ya kijamii kufuatia hali ya machafuko iliyotokea siku kadhaa zilizopita.

Lulu amelia na nchi ya Tanzania huku akisema Tanzania itusamehe kwakuwa tulichukulia kawaida mazuri ambayo nchi ilitupatia ikiwa ni pamoja na amani na mshikamano ambavyo kwa siku kadhaa zilizopita havikuonekana kabisa.

Wasanii wengi wamejitokeza kutoa salamu za pole kwa watu wote waliopoteza wapendwa wao katika machafuko hayo huku wakizidi kuombea kheri nchi yetu na kuzidi kuililia amani nchini Tanzania.